Quality Education for Quality Life

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

The appearance of administrative buildings, classrooms, assembly ground and a smartness gardens with beautiful flowers.

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

This is a place where scientific experiments are done.Science subject's teachers and students, meets here and learn by doing.It is a one among three rooms of new laboratories.

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

STAFF ROOM: All teachers meets here to relax,to do academic debates,to organize their daily activities related to their profession and planning on how to facilitate their youths (students).

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

AT CLASSROOM: students in the classroom, sitting calmly and confortably; responding to do the work as instructed and facilitated by their teeacher.

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

SIDE VIEW: other classrooms- buildings, assembly ground and gardens of beautiful flowers.

Sunday, December 11, 2016

MIAKA KUMI: TUNAKUMBUKA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE 2010 LUSHOTO SEKONDARI


Ilikuwa ni siku ya furaha iliyofana sana . . . ambapo kila mmoja alikuwa na tabasamu pana lililosawajika usoni mwake. Si wanafunzi . . . si wahitimu, wazazi, walimu, wageni na wanajamii waliojumuika katika mahafali hii, kila mmoja kwa nafasi yake aliweza kuonyesha furaha yake hasa kwa vijana walioandaliwa vyema wakiwa wanahitimu masomo yao na maisha yao shuleni yakifika tamati kwa mafanyikio. Siri kubwa ni nidhamu na tabia njema ya vijana hawa (wahitimu) ambayo ni kielelezo thabiti kwa kila mwanajumuiya wa lushoto sekondari wanajivunia.

KUMBUKUMBU YA MAHAFALI KIDATO CHA NNE (LUSHOTO SEKONDARI) 2014


Hii ni kumbukumbu ya mahafali ya kidato cha nne, shule ya sekondari lushoto; iliyofanyika tarehe 18 mwezi novemba, 2014. Kumbumbu hii inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka kumi (10) ya shule ya sekondari lushoto (tangu kuanzishwa mwaka 2006 hadi sasa mwaka 2016).

Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha na video; yaliyofana katika mahafali hii, ambayo yamebaki kuwa kumbukumbu na elimu tosha kwa wadau wa elimu na jamii kwa ujumla.

Monday, December 5, 2016

SIKIA KAZI NA WAJIBU WENU . . .




Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2016, wakiwa na mwalimu Juma Kimbute (JK) mapema leo hapa shuleni; dhumuni ni:


  • Kuwaasa kuendeleza tabia njema na nidhamu pindi watakapokuwa nyumbani / likizo.
  • Kuwapa shime kujisomea na kutafuta maarifa mapya yatakayokuwa na tija kwa kwaka wao wa masomo ujao.
  • Kuwakumbusha wanafunzi wajibu wao wakiwa shuleni na wakiwa nyumbani (muda wa likizo).
  • Kuwapangia kazi na zamu – wakati wa likizo ili kila mmoja ajitambue na atambue muda wake na kazi yake.







TUMEKUSIKIA ............TUTAZINGATIA . . . 👂👂👂







Saturday, October 29, 2016

KILA LA KHERI WATAHINIWA KIDATO CHA NNE 2016

Safari ya maisha ya kitaaluma ya vijana hawa.........naam inatariji kutia nanga punde wanapokwenda kuandika mitihani yao ya kuhitimu kidato cha nne Novemba mosi, 2016.

Thursday, September 1, 2016

TUKIO LA KUPATWA KWA JUA - WANAFUNZI NA WALIMU WASHUHUDIA

LEO Septemba Mosi 2016, wakati mamia ya watu wa mji wa Mbeya (Rujewa) wakishuhudia tukio la kupatwa kwa jua kwa karibu asilimia tisini na nane (98%), huku wilaya ya lushoto - tanga , hususani shule ya sekondari lushoto, wanafunzi na walimu pia walipata fursa hii adhimu ya kushuhudia tukio la kisayansi na kijiografia la kupatwa kwa jua.


Ilikuwa takribani majira ya saa tano hadi saa sita mchana, wasaa ambao kwa maeneo haya (shuleni) ndipo tukio hilo lilipata kuonekana, ingawaje lilisukwasukwa na wingi wa mawingu.







Tukio hili la kupatwa kwa jua, ni somo muhimu (kwa njia ya kushuhudia na kuona mubashara pasina shaka wala kuhadithiwa) walilopata kuona na kujifunza wanafunzi wetu, na kujiongezea maarifa Zaidi hasa katika somo la jiografia.

























Ikumbukwe kuwa tukio kama hilo la kupatwa kwa jua lilitokea Julai 31,1962 takribani miaka 50 iliyopita na tukio lingine lilitokea Aprili 18, 1977, na wataalamu wa anga wanabainisha kuwa tukio kama hilo litatokea tena hapa nchini Mei 21, 2031.

Sunday, August 14, 2016

HONGERA WALIMU WETU - KAZI NJEMA TWAWATAKIA

Jumuiya ya walimu, wanafunzi na wafanyakazi wote wa shule ya sekondari Lushoto, wana furaha kuwapongeza Mkuu wa shule Mr. Yona K. Ndekirwa na Madam Selestine Ifanda, kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa shule na kupangiwa vituo vyao vipya vya kazi.

WELCOME NEW LEADERS OF SCHOOL STUDENTS' GOVERNMENT [JULY 2016 - JULY 2017]

WELCOME NEW LEADERS OF SCHOOL STUDENTS' GOVERNMENT
[JULY 2016 – JULY 2017]
&
GOODBYE THE FORMER/ RETIRED LEADERS OF
[JULY 2015 – JULY 2016]

It's a regular, here at Lushoto Secondary School to exchange the phase of students’ government leadership. The appropriate time for new elections is always conducted at July on each year, where students use that opportunity to choose their leaders, who will lead and guide them in performing day to day school’ activities.

Saturday, July 30, 2016

JUMUIYA YA LUSHOTO SEKONDARI YAFANYA BARAZA LA SHULE

Siku ya tarehe 29 July 2016, ni siku ya pekee sana hasa kwa jumuiya ya lushoto sekondari inayojumuisha walimu, wafanyakazi wasio walimu na wanafunzi wote; ambapo walikutana kwa pamoja ili kujadiliana na kupanga mikakati dhidi ya kumpiga adui '' UJINGA na MWENENDO MBAYA'' hasa katika mustakabali mzima wa maisha ya kitaaluma.

JUMUIYA YA LUSHOTO SEKONDARI YAFANYA BARAZA LA SHULE

Siku ya tarehe 29 July 2016, ni siku ya pekee sana hasa kwa jumuiya ya lushoto sekondari inayojumuisha walimu, wafanyakazi wasio walimu na wanafunzi wote; ambapo walikutana kwa pamoja ili kujadiliana na kupanga mikakati dhidi ya kumpiga adui '' UJINGA na MWENENDO MBAYA'' hasa katika mustakabali mzima wa maisha ya kitaaluma.

Friday, June 24, 2016

ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2016

KUTOKA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO 

ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2016

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO JULAI MWAKA 2015

KUTOKA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO


MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO JULAI 2015






Friday, April 22, 2016

MIAKA 10 YA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO - MATUKIO NA KAZI MBALIMBALI ZIFANYIKAZO


MAJARIBIO YA KISAYANSI


Wanafunzi wakiwa pamoja na mwalimu magreth msangi, wakipata maelekezo kwa jinsi ya kufanya jaribio la kisayansi katika somo la baiolojia.


Wanafunzi wakiwa tayari kufanya na kuonyesha jaribio la kisayansi katika somo la kemia.


USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Kutunza mazingira ni wajibu muhimu katika mafunzo wayapatayo wanafunzi wawapo shuleni. Mazingira bora yenye kutunzwa, huvutia na kuongeza hamasa kwa wanafunzi kujivuna kuwepo mahali safi, salama na penye kuvutia.







ZIARA ZA KIMASOMO NJE YA SHULE NA NJE YA WILAYA YA LUSHOTO

Ni utaratibu wa shule kuratibu na kufanyikisha ziara za wanafunzi kimasomo ili kuwajengea fikra mpya na kujifunza zaidi ya kuwapo shuleni. Hivyo kila mwaka, wanafunzi hupata kutembelea maeneo mbalimbali kama vile mapango ya amboni -tanga, bahari ya hindi na bandari ya tanga, mbuga na hifadhi za taifa za wanyama pori na maeneo kadha wa kadha.












MAONYESHO YA KITAALUMA NA KAZI ZA UBUNIFU

Mbali na kujifunza darasani, mwanafunzi pia hupata fursa ya kuonyesha ubunifu na uwezo wa kutengeneza dhana mbalimbali za kitaaluma, baada ya kujifunza na kufahamu jambo fulani katika masomo yake.







Wanafunzi wakiwa katika mkusanyiko wa asubuhi, kwa ratiba za ukaguzi wa usafi na kupokea matangazo muhimu.








UTUNZAJI WA VITALU VYA MICHE NA KUPANDA MITI

Hapa shuleni wanafunzi wameweza kujifunza stadi za kimazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa vitalu ya miche, kuikuza na kuipanda ili kutunza uoto maridhawa kuzunguka maeneo ya eneo la shule.






MAFUNZO YA TEHAMA

Kutokana na uwepo wa vifaa vya kompyuta, imekuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi kujiunga katika klabu ( ICT – Skills Club) na kujifunza ujuzi mbalimbali na matumizi ya kompyuta na programu zake.











MIKUTANO YA KITAALUMA NA BARAZA LA SHULE

Kupitia mikutano hii na baraza, wanafunzi wanapata fursa nzuri ya kupata ushauri, nasaha za kitaaluma na nidhamu, kutunuku wanafunzi waliofanya vyema shuleni na pia kutambuana kila mdau na majukumu yake shuleni.









MIDAHALO YA LUGHA YA KISWAHILI NA KIINGEREZA


Mada hutolewa, wanafunzi nao hupata wasaa wa kujadili na kujiandaa kwa hoja za aidha kupinga ama kukubali hoja inayozungumziwa. Siku ya mdahalo huwa ni siku nzuri kwa wanafunzi, kwani ni fursa yao kuonyeshana umahili wa kujenga na kutetea hoja na hali ya kidato kimoja kushindana na kidato kingine. Huwa inavutia sana . . .