Quality Education for Quality Life

Sunday, December 11, 2016

KUMBUKUMBU YA MAHAFALI KIDATO CHA NNE (LUSHOTO SEKONDARI) 2014


Hii ni kumbukumbu ya mahafali ya kidato cha nne, shule ya sekondari lushoto; iliyofanyika tarehe 18 mwezi novemba, 2014. Kumbumbu hii inaenda sambamba na maadhimisho ya miaka kumi (10) ya shule ya sekondari lushoto (tangu kuanzishwa mwaka 2006 hadi sasa mwaka 2016).

Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha na video; yaliyofana katika mahafali hii, ambayo yamebaki kuwa kumbukumbu na elimu tosha kwa wadau wa elimu na jamii kwa ujumla.

Muonekano wa mazingira na majengo ya shule .........siku ya mahafali mwaka 2014

Mgeni rasmi (mkuu wa wilaya ya lushoto akiwasili shuleni siku ya mahafali
Mkuu wa wilaya ya lushoto, Mheshimiwa Majid Mwanga akipokewa na kukaribishwa shuleni katika mahafali ya kidato cha nne
Baadhi ya wazee waandamizi wa shule na kamati ya mahafali wakiwa ofisi ya mkuu wa shule kumpokea mgeni rasmi
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya, akisaini kitabu cha wageni


Mkuu wa shule Mr. Yona Ndekirwa akiambatana na mgeni rasmi na wageni wengine kumtembeza na kumwonyesha mazingira ya shule na majengo yake



KUTEMBELEA MAONYESHO YA KITAALUMA KATIKA CHUMBA CHA MAABARA



Mama Azali (mjumbe wa bodi ya shule) akiwa na wageni waalikwa ambao ni wakuu wa shule jirani za sekondari, ndani ya chumba cha maabara wakifuatilia kwa makini maonyesho ya kisayansi  yanayofanywa na wanafunzi



wanafunzi wakiwa makini kabisa katika vipimo na kufanyikisha majaribio ya kisayansi waliyoyaandaa na kuwaonyesha wageni waalikwa katika mahafali ya kidato cha nne.





KATIKA UWANJA WA MAHAFALI


Baadhi ya wanafunzi wahitimu wakiwa katika tabasamu bashasha . . .  kufuatilia kila tukio linalojili uwanjani

 Meza kuu: Mhe. Mkuu wa wilaya ya lushoto akiwa na Mhe. Shabani Omari Shekilindi (Bosnia)









Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wazazi waliojumuika pamoja katika mahafali hii




 Mzee Shamani akiwa na wasaa wa kutoa elimu na nasaha zake kwa wanafunzi waagwa na wahitimu


 Baadhi ya wanafunzi wahitimu







Meza kuu: Mkuu wa shule ya lushoto sekondari, Mr. Yona Ndekirwa

Meza kuu: kutoka kushoto ni Balozi Mshangama na Ndugu William Kusaga (mjumbe wa bodi ya shule)

Meza kuu: Mkuu wa wilaya ya lushosho, Mheshimiwa Majid Mwanga na Ndugu William Kusaga



Meza kuu: Ndugu William Kusaga, Mr. Yahaya (Afisa Elimu Taaluma Sekondari - lushoto) akiwa na wakuu wa shule ya Magamba S. S. na Shambalai S. S.


RISARA ILISOMWA KWA MGENI RASMI NA MUDA WA BURUDANI UKAWADIA

Risala: Dada Mkuu wa shule, akisoma risala ya wanafunzi wahitimu na masuala ya shule kwa mgeni rasmi


wanafunzi waaga (wanaobaki) nao hawakuwa nyuma. Walitumbuiza kwa nyimbo maridhawa kuwaaga dada na kaka zao



 Wenye vipaji vyao nao ........eeeeeeeh   walijitutumua katika kunywa soda kwa mtindo wa '' Tarumbeta'' ili kumpata bingwa wa zoezi hilo


 Kisha wasanii wa michezo ya  kuigiza na na kuchekesha wakarindima uwanjanina kutoa burudani yenye funzo ndani yake



NENO LA HEKIMA NA NASAHA ZA MGENI RASMI

Balozi Mshangama (mgeni rasmi) katika mahafali ya kidato cha nne 2014, akitoa nasaha zake kwa wahitimu na kujibu risala.

Katika harambee ya ujenzi wa maabara na majengo ya shule; Mhe. Shabani Omari Shekilindi (Bosnia) aliwaongoza vizuri wanajamii, wageni na wazazi ili kujitoa kwa hali na mali kufanyikisha ujenzi wa maabara. Akiwa ni kiongozi wa mfano, Mhe aliagiza shule kwenda kuchukua vifaa kadhaa vya ujenzi (ikiwa ni pamoja na saruji na bati)





WASAA WA KUTAMBUA JUHUDI ZA WANAFUNZI KITAALUMA, KUPONGEZA, KUTUNUKU VYETI NA ZAWADI MBALIMBALI

KWANZA WALIZAWADIWA WANAFUNZI WANAOBAKI AMBAO WALIONYESHA JUHUDI ZA KITAALUMA NA KUSHIKA NAFASI TATU BORA KATIKA VIDATO VYAO (MITIHANI YA NDANI)
















WAKAFUATA WAHITIMU KUTUNUKIWA VYETI NA ZAWADI







ZAWADI ZA SHULE  KWA WAGENI KATIKA SHUKRANI NA KUTAMBUA MCHANGO WA WAGENI HAO KATIKA MAENDELEO YA SHULE HII

Ndugu William Kusaga (mjumbe bodi ya shule) akishuhudiwa na mkuu wa shule Mr. Yona Ndekirwa,  akikabidhi zawadi kwa Balozi Mshangama

Ndugu William Kusaga (mjumbe bodi ya shule) akiwa na Balozi Mshangama; kwa pamoja wakimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya lushoto Mhe. Majid Mwanga.

0 comments:

Post a Comment