Quality Education for Quality Life

Friday, February 5, 2016

KUMBUKUMBU YA MAHAFALI YA KWANZA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO 2009

Mahafali ya kwanza kufanyika katika shule ya sekondari Lushoto, ikiwa chini ya uongozi wa mkuu wa shule (Late) Mama Ester Mapunda.

Mahafali haya ni wanafunzi wa kwanza ambao walianza kidato cha kwanza mwaka 2006 wakati ambao shule hii ilianza. Hivyo ni mahafali pekee tena yenye kumbukumbu nzuri inayoonyesha wapi shule ilianza, wadau mahususi wapi (walimu, wanafunzi na wadau wa maendeleo wa shule hii) waliokuwepo wasaa huo na ni kwa hali ipi na changamoto zipi zilikuwapo muda huo................


Sherehe hizi za Mahafari kidato cha nne 2009, zilihudhuriwa na mgeni rasmi; ambaye ni mkuu wa wilaya ya lushoto (wakati huo - 2009), Mheshimiwa Sophia Mjema akiambatana na mheshimiwa Katuimu tawala wa wilaya ya lushoto na wajumbe wengine muhimu.

MAONYESHO YA KITAALUMA YALIYOFANYWA NA WAHITIMU WENYEWE


Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne 2009, wakionyesha majaribio ya kisayansi katika somo la fizikia

Wahitimu wa kidato cha nne 2009, wakionyesha hatua mbalimbali za mmomonyoko wa udongo katika mto tangu chanzo cha maji hadi hatua ya mwisho mto unapomwaga maji yake baharini; katika somo la jiografia.


Katika maandalizi ya kufanyikisha mahafali hii, vijana wa lushoto sekondari (wa vidato vya chini) nao hawakuwa nyuma kuwaaga kaka na dada zao; walijituma kuaanda kwa kadri walivyogawana majukumu na vitengo mbalimbali.

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne 2009; mapema asubuhi siku ya mahafali, wakiwa katika picha ya pamoja.

MAPOKEZI YA MGENI RASMI WA MAHAFALI KIDATO CHA NNE 2009


Ndugu Mkuu wa shule (Late) Mama Ester Mapunda akimpokea na kumkaribisha katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne - lushoto sekondari, Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema.

Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema, akiwasalimia wageni waambata katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne - lushoto sekondari.

Akiwa katika ofisi ya mkuu wa shule: Ndugu Mkuu wa shule (Late) Mama Ester Mapunda akitoa utambulisho na neno la kumkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne - lushoto sekondari.




Ndugu Mkuu wa shule (Late) Mama Ester Mapunda akiambatana na wajumbe wa bodi na wageni waalikwa, akimpa maelezo mafupi Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema; kuhusu maendeleo ya shule ya sekondari lushoto na miradi yake ya ujenzi, muda mfupi kabla ya kuingia katika uwanja wa mahafali.


Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema, akiwasalimia wahitimu wa kidato cha nne 2009


KATIKA UWANJA WA MAHAFALI KIDATO CHA NNE- SHEREHE IMEANZA

Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema, akiwasili kataka uwanja wa mahafari huku akiambatana na Mkuu wa shule (Late) Mama Ester Mapunda na Mwenyekiti wa kijiji - Yoghoi; Mr Tullo.

Kwa furaha na bashasha, wahitimu wa kidato cha nne 2009, wakiingia kwa mbwembwe na madaha na kupokewa na Mgeni rasmi katika uwanja wa mahafali tayari kuanza sherehe.

Wakiwa na nyuso za tabasamu, wahitimu wa kidato cha nne wakifuatilia kwa makini jinsi burudani za  mahafali na shughuli nyinginezo zikiendelea uwanjani hapo.

Baadhi ya wageni waalikwa, wakiwapo walimu, wazazi na walimu wa shule jirani na rafiki walioalikwa kuhudhuria sherehe za mahafali kidato cha nne 2009.

Nasaha na dua za kufungua sherehe za mahafali kidato cha nne.

Risala ya waagwa kwa mgeni rasmi pia ilitolewa.

BURUDANI ZA MAHAFARI KIDATO CHA NNE 2009

Wahitimu nao hawakukubali kuwa nyuma, walijipanga na kutoa burudani nzito ya "RAP" (muziki wa kufokafoka) uliowainua wahudhuriaji vitini na kushangilia kwa furaha.






Ndugu Mkuu wa shule (Late) Mama Ester Mapunda akimkaribisha Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema, kuzungumza na wahitimu na wageni waalikwa wote katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne - lushoto sekondari.

Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya Lushoto , Mheshimiwa Sophia Mjema, akiakihutubia na kutoa ujumbe wake maalum kwa wahitimu na hadhira yote iliyohudhuria uwajani hapo katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne - lushoto sekondari.


MUDA WA KUTUNUKU VYETI NA ZAWADI KWA WAHITIMU







PICHA ZA PAMOJA ZA MEZA KUU NA WAHITIMU KIDATO CHA NNE 2009
























0 comments:

Post a Comment