Quality Education for Quality Life

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

The appearance of administrative buildings, classrooms, assembly ground and a smartness gardens with beautiful flowers.

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

This is a place where scientific experiments are done.Science subject's teachers and students, meets here and learn by doing.It is a one among three rooms of new laboratories.

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

STAFF ROOM: All teachers meets here to relax,to do academic debates,to organize their daily activities related to their profession and planning on how to facilitate their youths (students).

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

AT CLASSROOM: students in the classroom, sitting calmly and confortably; responding to do the work as instructed and facilitated by their teeacher.

QUALITY EDUCATION FOR QUALITY LIFE

SIDE VIEW: other classrooms- buildings, assembly ground and gardens of beautiful flowers.

Friday, April 22, 2016

MIAKA 10 YA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO - MATUKIO NA KAZI MBALIMBALI ZIFANYIKAZO


MAJARIBIO YA KISAYANSI


Wanafunzi wakiwa pamoja na mwalimu magreth msangi, wakipata maelekezo kwa jinsi ya kufanya jaribio la kisayansi katika somo la baiolojia.


Wanafunzi wakiwa tayari kufanya na kuonyesha jaribio la kisayansi katika somo la kemia.


USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Kutunza mazingira ni wajibu muhimu katika mafunzo wayapatayo wanafunzi wawapo shuleni. Mazingira bora yenye kutunzwa, huvutia na kuongeza hamasa kwa wanafunzi kujivuna kuwepo mahali safi, salama na penye kuvutia.







ZIARA ZA KIMASOMO NJE YA SHULE NA NJE YA WILAYA YA LUSHOTO

Ni utaratibu wa shule kuratibu na kufanyikisha ziara za wanafunzi kimasomo ili kuwajengea fikra mpya na kujifunza zaidi ya kuwapo shuleni. Hivyo kila mwaka, wanafunzi hupata kutembelea maeneo mbalimbali kama vile mapango ya amboni -tanga, bahari ya hindi na bandari ya tanga, mbuga na hifadhi za taifa za wanyama pori na maeneo kadha wa kadha.












MAONYESHO YA KITAALUMA NA KAZI ZA UBUNIFU

Mbali na kujifunza darasani, mwanafunzi pia hupata fursa ya kuonyesha ubunifu na uwezo wa kutengeneza dhana mbalimbali za kitaaluma, baada ya kujifunza na kufahamu jambo fulani katika masomo yake.







Wanafunzi wakiwa katika mkusanyiko wa asubuhi, kwa ratiba za ukaguzi wa usafi na kupokea matangazo muhimu.








UTUNZAJI WA VITALU VYA MICHE NA KUPANDA MITI

Hapa shuleni wanafunzi wameweza kujifunza stadi za kimazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa vitalu ya miche, kuikuza na kuipanda ili kutunza uoto maridhawa kuzunguka maeneo ya eneo la shule.






MAFUNZO YA TEHAMA

Kutokana na uwepo wa vifaa vya kompyuta, imekuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi kujiunga katika klabu ( ICT – Skills Club) na kujifunza ujuzi mbalimbali na matumizi ya kompyuta na programu zake.











MIKUTANO YA KITAALUMA NA BARAZA LA SHULE

Kupitia mikutano hii na baraza, wanafunzi wanapata fursa nzuri ya kupata ushauri, nasaha za kitaaluma na nidhamu, kutunuku wanafunzi waliofanya vyema shuleni na pia kutambuana kila mdau na majukumu yake shuleni.









MIDAHALO YA LUGHA YA KISWAHILI NA KIINGEREZA


Mada hutolewa, wanafunzi nao hupata wasaa wa kujadili na kujiandaa kwa hoja za aidha kupinga ama kukubali hoja inayozungumziwa. Siku ya mdahalo huwa ni siku nzuri kwa wanafunzi, kwani ni fursa yao kuonyeshana umahili wa kujenga na kutetea hoja na hali ya kidato kimoja kushindana na kidato kingine. Huwa inavutia sana . . .