MAJARIBIO YA KISAYANSI
Wanafunzi wakiwa pamoja na mwalimu magreth msangi, wakipata maelekezo kwa jinsi ya kufanya jaribio la kisayansi katika somo la baiolojia.
Wanafunzi wakiwa tayari kufanya na
kuonyesha jaribio la kisayansi katika somo la kemia.
USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Kutunza mazingira ni wajibu muhimu
katika mafunzo wayapatayo wanafunzi wawapo shuleni. Mazingira bora
yenye kutunzwa, huvutia na kuongeza hamasa kwa wanafunzi kujivuna
kuwepo mahali safi, salama na penye kuvutia.
ZIARA ZA KIMASOMO NJE YA SHULE NA NJE
YA WILAYA YA LUSHOTO
Ni utaratibu wa shule kuratibu na
kufanyikisha ziara za wanafunzi kimasomo ili kuwajengea fikra mpya na
kujifunza zaidi ya kuwapo shuleni. Hivyo kila mwaka, wanafunzi hupata
kutembelea maeneo mbalimbali kama vile mapango ya amboni -tanga,
bahari ya hindi na bandari ya tanga, mbuga na hifadhi za taifa za
wanyama pori na maeneo kadha wa kadha.
MAONYESHO YA KITAALUMA NA KAZI ZA
UBUNIFU
Mbali na kujifunza darasani, mwanafunzi
pia hupata fursa ya kuonyesha ubunifu na uwezo wa kutengeneza dhana
mbalimbali za kitaaluma, baada ya kujifunza na kufahamu jambo fulani
katika masomo yake.
Wanafunzi wakiwa katika mkusanyiko wa
asubuhi, kwa ratiba za ukaguzi wa usafi na kupokea matangazo muhimu.
UTUNZAJI WA VITALU VYA MICHE NA KUPANDA
MITI
Hapa shuleni wanafunzi wameweza
kujifunza stadi za kimazingira ikiwa ni pamoja na kuandaa vitalu ya
miche, kuikuza na kuipanda ili kutunza uoto maridhawa kuzunguka
maeneo ya eneo la shule.
MAFUNZO YA TEHAMA
Kutokana na uwepo wa vifaa vya
kompyuta, imekuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi kujiunga katika
klabu ( ICT – Skills Club) na kujifunza ujuzi mbalimbali na
matumizi ya kompyuta na programu zake.
MIKUTANO YA KITAALUMA NA BARAZA LA
SHULE
Kupitia mikutano hii na baraza,
wanafunzi wanapata fursa nzuri ya kupata ushauri, nasaha za kitaaluma
na nidhamu, kutunuku wanafunzi waliofanya vyema shuleni na pia
kutambuana kila mdau na majukumu yake shuleni.
MIDAHALO YA LUGHA YA KISWAHILI NA
KIINGEREZA
Mada hutolewa, wanafunzi nao hupata
wasaa wa kujadili na kujiandaa kwa hoja za aidha kupinga ama kukubali
hoja inayozungumziwa. Siku ya mdahalo huwa ni siku nzuri kwa
wanafunzi, kwani ni fursa yao kuonyeshana umahili wa kujenga na
kutetea hoja na hali ya kidato kimoja kushindana na kidato kingine.
Huwa inavutia sana . . .
0 comments:
Post a Comment