Quality Education for Quality Life

Sunday, December 11, 2016

MIAKA KUMI: TUNAKUMBUKA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE 2010 LUSHOTO SEKONDARI


Ilikuwa ni siku ya furaha iliyofana sana . . . ambapo kila mmoja alikuwa na tabasamu pana lililosawajika usoni mwake. Si wanafunzi . . . si wahitimu, wazazi, walimu, wageni na wanajamii waliojumuika katika mahafali hii, kila mmoja kwa nafasi yake aliweza kuonyesha furaha yake hasa kwa vijana walioandaliwa vyema wakiwa wanahitimu masomo yao na maisha yao shuleni yakifika tamati kwa mafanyikio. Siri kubwa ni nidhamu na tabia njema ya vijana hawa (wahitimu) ambayo ni kielelezo thabiti kwa kila mwanajumuiya wa lushoto sekondari wanajivunia.

Mwaka 2010 shulu iliweza kuwafanyia mahafali jumla ya wahitimu 138 wasichana wakiwa 64 na wavulana 74. Wanafunzi wahitimu wakiwa na viongozi wao (serikali ya wanafunzi):-
  • Kaka Mkuu - Rashidi M. Shunda
  • Dada Mkuu - Paulina C. Sengasu
  • Katibu Mkuu - Peter M. Mbwambo

Wanafunzi wahitimu wakiimba kwa furaha kusherehesha mahafali yao kabla ya kwenda uwanja wa mahafali ulioandaliwa.

Meza kuu: ikisheheni wazee (akiwamo Mzee Habibu - Mwenyekiti wa kamati wazazi ), mgeni rasmi na mkuu wa shule.

 Mwandamizi kamati ya mahafali, Mama Kiondo akitoa tarifa fupi hukusu maandalizi na mahafali yenyewe kwa ujumla


Wahitimu wakiimba wimbo wa shule na nyimbo maalumu ya mahafali

Mzee Imamu Hussein Shedafa (Mzazi rasmi wa mahafali) akitoa neon na dua kuombea shughuli ya mahafali.



wahitimu kidato cha nne wakionekana watulivu na makini sana

 risala: Dada mkuu Paulina C Sengasu na Katibu wa serikali ya wanafunzi, Peter M. Mbwambo wakisoma risala kwa mgeni rasmi siku ya mahafali yao 2010


Baada ya kusomwa na kukabidhiwa risala kwa mgeni rasmi; wanafunzi waliburudika kwa nyimbo ya mziki wa miondoko ya ''Kufoka-foka (rap)'' kwa jina la Upesi - Upesi . . . aaaahhh👊👊









 mgeni rasmi akitoa hotuba yake kwa wahitimu, wageni, wanafunzi wanaobaki na jumuiya yote ya lushoto sekondari

 meza kuu: kutoka kulia ni Ndugu mgeni rasmi (toka tanga sement) akiwa na mkewe, mkuu wa shule na mwalimu wa taaluma.

 mwalimu wa taaluma Mr. Mapengele B. C. akitoa mwongozo na utaratibu wa meza kuu



wanafunzi wahitimu wakitunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali

 mkuu  wa shule Mr. Yona Ndekirwa akikabidhi zawadi ya shule na jumuiya ya watu wa lushoto sekondari kwa mgeni rasmi mara baada ya zoezi la kutunuku wahitimu vyeti na zawadi



zawadi mbuzi akikabidhiwa kwa mgeni rasmi kuwa shukrani kwa mchango wake kwa maendeleo ya shule.


 mkuu wa shule akiongoza msafara wa mgeni rasmi kutoka katika uwanja wa mahafali baada ya kuhitimisha shughuli hiyo ya kitaaluma





 Baada ya sherehe ya mahafali kufika tamati


 Wahitimu kidato cha nne 2010




0 comments:

Post a Comment