Katika kuadhimisha wiki
ya sheria nchini tanzania, wilaya ya lushoto na uongozi mzima ngazi
ya mahakama ya lushoto; walipata wasaa wa kutembelea jumuiya ya
sekondari ya lushoto.
Dhumuni kubwa
linaloambatana na ziara hiyo ni kutoa elimu na msaada wa kisheria kwa
jamii hasa wanafunzi (kundi la vijana na watoto) ambalo kwa kiasi
kikubwa ni walengwa na waathirika dhidi ya makosa ya jinai, mambo ya
mirathi, unyanyasaji wa kijinsia, ajira na mimba za utotoni. Aidha,
ziara hii imelenga pia kutoa mafunzo na ukaribisho wa wenye uhitaji
wa msaada wa kisheria kabla na wakati wapatapo matatizo ya kisheria.
Hakimu wa Mahakama ya Lushoto -Mhe. N.
R. Mwaseba (Mama Mwaseba), akitoa utangulizi wa mafunzo na utoaji elimu juu ya masuala ya kisheria, walipowatembelea wanafunzi wa Lushoto Sekondari.
|
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Lushoto -
Mhe. Catherine madili akitoa elimu juu ya haki na wajibu wa mtoto.
|
Wiki hii ya sheria (kwa
mwaka huu wa sheria) inaadhimishwa kwa kauli mbiu inayolenga mhimili
wa mahakama na vyombo vyake kuweza kuhudumia jamii kisheria kwa
haraka na ufanisi zaidi, ili kuiwezesha jamii husika kurejea katika
shughuli za ujenzi wa uchumi na taifa kwa ujumla.
Wanafunzi (pichani) wakifuatilia na kusikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizowasilishwa, katika maadhimisho ya wiki ya sheria hapa Lushoto Sekondari. |
Wanafunzi wa lushoto
sekondari, waliandaliwa kupata mafunzo (elimu) juu ya :-
- Mahakama na muundo wake
- Sheria za nchi
- Haki na wajibu wa mtoto
- Makosa ya jinai na uhaini
- Sheria ya mirathi na sifa za warithi
- Mapenzi na mimba za utotoni – sheria inasemaje?
- Sifa za wosia
Mwisho wa semina
(mafundisho) hayo, wanafunzi na walimu walipata nafasi ya kuuliza
maswali mbalimbali yanayohusiana na wigo wa kisheria ili kupata
ufafanuzi, tafasili sahihi, mwongozo na muhafaka kwa masuala
tatanishi kisheria.
Wanafunzi na jumuiya ya
walimu wa sekondari ya lushoto, walishukuru na kuonyesha furaha yao
kwa ziara hii iliyowapa elimu pana katika masuala sheria.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne (ambao ni washiriki wa mafunzo) wakiwa katika picha ya pamoja walimu na wageni (Waheshimiwa Mahakimu - Mahakama ya Lushoto), mara baada ya kupata mafunzo/elimu. |
0 comments:
Post a Comment