Quality Education for Quality Life

Saturday, July 30, 2016

JUMUIYA YA LUSHOTO SEKONDARI YAFANYA BARAZA LA SHULE

Siku ya tarehe 29 July 2016, ni siku ya pekee sana hasa kwa jumuiya ya lushoto sekondari inayojumuisha walimu, wafanyakazi wasio walimu na wanafunzi wote; ambapo walikutana kwa pamoja ili kujadiliana na kupanga mikakati dhidi ya kumpiga adui '' UJINGA na MWENENDO MBAYA'' hasa katika mustakabali mzima wa maisha ya kitaaluma.


Wanafunzi wakiwa katika utulivu kusikiliza, kuchangia na kujadili mada mbalimbali za baraza la shule.

Akiwa ni mwalimu wa zamu wa wiki, mwalimu mwandamizi msaidizi wa nidhamu, Mr. Godfrey Mwasenga, aliongoza shughuli nzima ya baraza la shule, kwa umahili mkubwa na uliotiririka kwa mpangilio wa tukio kwa tukio.
Mwalimu Godifrey Mwasenga akitoa utaratibu wa kufanyika kwa baraza la shule kwa wanafunzi.













Katika utangulizi wa baraza la shule, wanafunzi kadhaa waliweza kutumbuiza na kunogesha shughuli hii kwa kuweza kuimba na kughani mashairi kwa mtindo wa '' mziki wa kufokafoka - Hip hop'' na kuweza kuwapa wajumbe wote mkao wa tayari kuanza baraza.




Baraza hili lilihudhuriwa na kufunguliwa na mkuu wa shule, Mr. Yona Ndekirwa na kuratibiwa vizuri na mwalimu mwandamizi wa taaluma, Mr. Swalehe A. Msangi.
Mkuu wa shule , Mr Yona Ndekirwa akitoa mwongozo, nasaha na neon la ufunguzi wa baraza la shule.

Kadhalika, waliohudhuria pia ni pamoja na walimu wote, viongozi serikali ya wanafunzi (2015 -- 2016) na wanafunzi wote (kidato cha kwanza hadi kidato cha nne).

Kutoka kushoto, ni dada mkuu , kaka mkuu, katibu wa serikari ya wanafunzi na mwanafunzi mlezi wa wanafunzi wa kike (matron)



Wanafunzi walipata wasaa na fursa ya kuuliza juu ya mambo kadha wa kadha yahusuyo taaluma, nidhamu, michezo, uongozi na kadhalika.








Pia waliweza kutoa ushauri, maoni na mapendekezo ya nini kifanyike ili kukuza na kuboresha mazingira yao ya kujifunzia.

Vile vile katika baraza hili, walimu walipata fursa adhimu ya kusikia kutoka kwa wanafunzi wao, na kuwa mrejesho wa kazi zao za kila siku na jinsi gani zimepokewa na wanafunzi wao.

Ikiwa ni agenda mojawapo katika baraza la shule, wanafunzi wa vidato vyote (I,II,III na IV) waliofanya vizuri katika mitihani yao ya nusu mhula (June 2016), walipongezwa na kutambulishwa kwa wanafunzi wenzao.

Mbali Zaidi, waliopata kushika nafasi za juu katika ufaulu (yaani nafasi tatu za juu za ufaulu), walipongezwa Zaidi na kuzawadiwa zawadi mbalimbali ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wao, juhudi zao na kuwatia moyo ili wafanye vizuri Zaidi, pia kuwapa hamasa na wengine kujibidiisha ili kuwa na mafanyikio kama wenzao waliofanya vizuri.
Wanafunzi wa kidato cha nne 2016, waliofungana kwa kushika nafasi ya pili kwa ufaulu, wakiwa meza kuu kupokea zawadi zao.


Mwanafunzi wa kidato cha ne 2016, Zawadi akipokea zawadi yake ya kufaulu na kushika nafasi ya tatu.




Mwanafunzi wa kidato cha nne 2016, Atiki Shelimo akipokea zawadi yake kwa kufaulu na kushika nafasi ya kwanza.

Ni imani kuwa, kwa baraza hili wanafunzi watakuwa wamepata ufumbuzi wa masuala yaliyokuwa yakiwatatiza na kuzingatia mawaidha yote waliyopewa na kuwa wanafunzi bora. 
Mwalimu mwandamizi taaluma, Mr Swalehe A. Msangi akisisitiza jambo kwa wanafunzi kuhusu taaluma.

Lushoto Sekondari  -- Elimu bora kwa Maisha bora



0 comments:

Post a Comment