Ilikuwa takribani majira ya saa tano hadi saa sita mchana, wasaa ambao kwa maeneo haya (shuleni) ndipo tukio hilo lilipata kuonekana, ingawaje lilisukwasukwa na wingi wa mawingu.
Tukio hili la kupatwa kwa jua, ni somo muhimu (kwa njia ya kushuhudia na kuona mubashara pasina shaka wala kuhadithiwa) walilopata kuona na kujifunza wanafunzi wetu, na kujiongezea maarifa Zaidi hasa katika somo la jiografia.
Ikumbukwe kuwa tukio kama hilo la kupatwa kwa jua lilitokea Julai 31,1962 takribani miaka 50 iliyopita na tukio lingine lilitokea Aprili 18, 1977, na wataalamu wa anga wanabainisha kuwa tukio kama hilo litatokea tena hapa nchini Mei 21, 2031.
0 comments:
Post a Comment