Quality Education for Quality Life

Sunday, January 10, 2016

MIAKA KUMI TIMILIFU YA UHAI NA MAFANIKIO YA SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO



Ni takribani miaka kumi sasa tangu yalipofanyika maamuzi ya hekma na busara yaliyojali maslahi ya wengi hasa kizazi kilichopo na vizazi vijavyo. Pengine tunaweza kufikiri na kusema kuwa wadau walioanzisha shule hii, huenda walizungumza maneno haya:

". . .  jamani yafaa katika kata yetu . . . tuwe na shule ya sekondari . . . "
". . . sawa ni wazo zuri, .........mimi naliunga mkono wazo hilo . . . "
". . . . ila eneo la kujenga hiyo shule ni wapi ? . . . maaana hatuna eneo hapa"
". . . . .hapana, kwa maana tunayo nia na dhamira basi eneo litapatikana"
". . . . kweli tukitoa visehemu vya maeneo yetu na kijiji kusimamia hili, tutapata eneo"

. . . ni mengi mno yaliyofanyika na kuzungumzwa, ila yote yalilenga nia na dhamira moja tu........kuwa na shule ya sekondari lushoto katika kata yao, kijiji cha yoghoi - mshuza.
Masaa, siku hatimaye miezi ilikatika huku watu hao wakihamasishana na kujitoa kwa hali na mali wakatafuta eneo, wakaanza ujenzi, chumba kimoja hadi kingine hata kukamilisha majengo muhimu ya vyumba vya madarasa vya awali, jengo la utawala na vyoo. 
Kadhalika selikari nayo haikuwa nyuma, bali iliunga mkono jitihada hizo kwa kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia . . . walengwa nao wakafika kukamilisha dhamira hii nao si wengine ila ni wanafunzi, walimu na wadau wengine wa shule hii.
 Kwa pamoja walijitoa na kila mmoja kutimiza jukumu lake.
Ustawi ukaanza kuonekana, jamii ikajivunia kwa lengo na dhamira yao kuanza kutimia. 
Ni jambo la kheri sana, haikuwa kazi rahisi, ila ni kazi iliyoitaji moyo na uvumilivu.
Tangu mwezi mei 2006 hadi sasa mwaka 2016; ni miaka kumi imetimia.
 Jumuiya ya watu,wanafunzi, walimu, wafanyakazi, wazazi na wadau wengine, wana kila sababu ya kujivunia umri huu na furaha hii adhimu ya taasisi kutimiza miaka kumi ya mafanyikio, mwangaza na  maendeleo.

 Hongera Shule ya Sekondari Lushoto



Tuna kutakia kheri ukue na kuendelea kuhudumia jamii yako zaidi na zaidi tena ukiendelea kitaalamu zaidi kuandaa na kufunza vijana wako.

0 comments:

Post a Comment