Mkulima huwa na furaha
awajibikapo katika hatua zote za kilimo tangu kuandaa shamba /
bustani, mbegu, kupanda, kutunza na kukuza mimea yake iwe katika
ubora unaostahili; aidha furaha zaidi huwa wakati wa mavuno, kutumia
ama kuuza kwa tija.
Hali hii haijifichi
miongoni mwa wanafunzi – wanakikundi wa elimu ya kujitegemea (EK)
na uzalishaji mali wa hapa shuleni. Kwa nyakati tofauti mbali na
vipindi vyao vya darasani, pia wanafunzi hupata fursa ya kujifunza na
kushiriki shughuli za ujasilia mali kwa vitendo.
Sasa ni wakati wa mazumo
na mauzo, baada ya shughuli mbalimbali za upandaji, ukuzaji na
utunzaji wa bustani. Mavumo yapatikanayo, uweza kugawiwa kwa
wanafunzi na wanakikundi ama kuuzwa na fedha ipatikanayo kuweza
kusaidia baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji wa vifaa ya kujifunzia
kama vile kununua madaftali, kalamu na nyakati nyingine fedha hizo
hutumika kununua mbegu, madawa na vifaa vya bustanini kama vile
mipira ya maji (kumwagilia), ndoo / madumu ya maji, nk.
Vijana hufurahia sana
elimu hii shirikishi ya wakiwa darasani na wakiwa nje ya darasa kwa
kazi za ujuzi zaidi.
0 comments:
Post a Comment