Pages

Sunday, August 14, 2016

HONGERA WALIMU WETU - KAZI NJEMA TWAWATAKIA

Jumuiya ya walimu, wanafunzi na wafanyakazi wote wa shule ya sekondari Lushoto, wana furaha kuwapongeza Mkuu wa shule Mr. Yona K. Ndekirwa na Madam Selestine Ifanda, kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa shule na kupangiwa vituo vyao vipya vya kazi.


Kwa fursa hii, jumuiya ya sekondari Lushoto, inawapongeza na kuwatakia kazi njema yenye kupigiwa mfano, yenye kuleta tija na ustawi katika taaluma na maendeleo kwa ujumla.

Tunaamini, ingawaje walimu wetu watakuwa mbali nasi, bado mchango na jitihada zao katika taaluma tutazienzi, kuzithamini na kuzitunza kwa jamii ya sasa na ya baadaye.

Sanjari na kuwapongeza walimu wetu na kuwaaga kwa hafla fupi iliyofanyika hapa shuleni, pia jumuiya ya Lushoto sekondari ina furaha kumpokea na kumkaribisha mkuu mpya wa shule Mr. P. B. Shauri, ambaye naye amepata fursa ya kupangiwa kituo kipya cha kazi - Lushoto sekondari.

Ili kuleta ufanisi katika kazi, jumuiya ya wanaLushoto sekondari hukumbuka maneno yafuatayo, ili kurudisha hari, moyo na kutia bidii Zaidi katika kufanya kazi, kwani mwalimu hufanya kazi popote kwa mazingira yoyote na kuisaidia jamii yake kumpiga vita adui ujinga na umasikini.


'' Luck follows hard working people

That's the way you've earned that promotion

Congratulations on your new role . . . We are proud of you

May your new assignment . . . 'Be exciting and heart fulfilling ''

Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha, yakitanguliwa na mkuu wa shule Mr. Yona K. Ndekirwa akiagana na wanafunzi, Mkuu mpya wa shule Mr. P.B. Shauri akisalimiana na wanafunzi na hafla fupi ya kuwaaga walimu.

Wanafunzi wakiwa wamekusanyika na kuwasikiliza walimu wakiwapa matangazo na salamu mbalimbali .

Mkuu wa shule Mr. Yona K. Ndekirwa, akiagana na wanafunzi wa Lushoto sekondari kwa kuwanasihi kujibidiisha katika taaluma na nidhamu wawapo shuleni.














Mkuu mpya wa shule Mr. P. B. Shauri akiwasilimu wanafunzi, na kuwapa miongozo na maelekezo juu ya taratibu za shule, uwajibikaji wa kazi za kila siku za wanafunzi na majukumu ya baadhi ya wanafunzi (madarasa ya mitihani - kidato cha pili na nne) kila siku asubuhi wafikapo shuleni.







Hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga walimu (Mr. Yona Ndekirwa na Madam Selestina Ifanda)

Hafla ilianza kwa kupiga picha ya pamoja ikijumuisha Mkuu wa shule (Anayeagwa) Mr. Yona Ndekirwa akiambatana na mkewe, Mkuu wa shule ya msingi Yoghoi, Mama Mariam Sengasu, wajumbe wa bodi ya shule, walimu wote wa lushoto sekondari pamoja na walimu toka chuo kikuu cha Dar es Salaam.



Ratiba ya chakula na vinywaji ilifuata, baadhi ya wahusika wa hafla hii wakijipatia chakula na kuingia mahala husika.

MC wa hafla, Mr Godfey Mwasenga akitoa utangulizi mfupi na jinsi gani ataiongoza hii hafla.

Makamu mkuu wa shule Mama Beatrice Shemmela, akifungua hafla hii kwa neon la shukrani, pongezi na nasaha kwa walimu wanaondoka na wanaobaki . . . kujibidiisha katika kazi Zaidi na kuangalia maslahi mapana ya kitaaluma.
Mkuu wa shule ya msingi - Yoghoi, Mama Mariam Sengasu akitoa shukrani, pongezi na nasaha kwa walimu jinsi ya kuishi na kufanya kazi katika mazingira anuai, na kuleta tija.
Mwenyekiti wa kijiji - Yoghoi, Ndugu Kadala akitoa kongole kwa walimu waagwa na kuwatakia kazi njema yenye mafanyikio Zaidi.
Mwenyekiti wa mfuko wa kijamii - lushoto sekondari, Mr. Kabelwa akiambatana na Makamu mkuu wa shule, Mama Beatrice Shemmela, kwa niaba ya jumuiya ya shule wakitoa pongezi na zawadi kwa Mkuu wa shule (muagwa) Mr. Yona Ndekirwa. 
Mwenyekiti wa mfuko wa kijamii - lushoto sekondari, Mr. Kabelwa akiambatana tena na Makamu mkuu wa shule, Mama Beatrice Shemmela, kwa niaba ya jumuiya ya shule wakitoa pongezi na zawadi kwa mwalimu (muagwa) Madam Selestina Ifanda. 
Mkuu wa shule mteule (kituo kipya cha kazi na mwalimu muagwa), Mdam Selestina Ifanda akitoa neon la shukrani kwa jumuiya yote ya lushoto sekondari na kuwanasihi kufanya kazi kwa juhudi na maarifa Zaidi.


Mkuu wa shule (muagwa) Mr. Yona Ndekirwa akitoa shukrani kwa ushirikiano na mshikamano alioupata akiwa na jumuiya ya lushoto sekondari, na kuwahaidi kushirikiana nao Zaidi na Zaidi.

MC wa shughuli hii, Mr. Godfrey Mwasenga akiitimisha hafla hii kwa maneno machache na sala.

Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla, kutoka kulia ni Mzee kadala (mwenyekiti wa kijiji - Yoghoi), Mzee Mkonyi (Mjumbe wa bodi ya shule) na Mama Mbaga (Mkuu wa shule mstaafu - shule ya msingi Yoghoi).








Mr. P.B. SHAURI
Madam SELESTINA IFANDA
Mr. YONA NDEKIRWA


Congratulations on your job promotion!
We wish all the success on your next endeavor.

No comments:

Post a Comment